Saturday, March 22, 2014


Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Ooo…Nooo! Wakati hati ya kifo cha aliyekuwa rapa bora Bongo, marehemu Albert Keneth Mangweha ‘Ngwea’, ikiendelea kushikiliwa nchini Afrika Kusini alikokutwa na umauti mwaka jana, kwenye kaburi lake kumekutwa tunguli zilizozungushiwa sanda,Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Monica, Kihonda mkoani Morogoro, Octavian Msimbe akionyesha tunguli zilizozungushiwa sanda zilizokutwa kaburini kwa marehemu Ngwea.
Tunguli hizo zilikutwa Ijumaa ya wiki iliyopita na Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Monica, Kihonda mkoani Morogoro, Octavian Msimbe ambapo ziliibua hofu miongoni mwa waumini wa kanisa hilo lililopo katika eneo hilo la makaburi.
Marehemu Albert Keneth Mangweha ‘Ngwea’.
PADRI AKEMEA
Awali, ilielezwa kuwa siku hiyo padri huyo alioteshwa ndoto usiku juu ya uwepo wa vitu vya ajabu katika makaburi hayo ndipo akakemea kabla ya kwenda kuvishuhudia asubuhi yake (Ijumaa iliyopita) huku paparazi wetu akinyetishiwa na kuwahi eneo la tukio.
PAPARAZI USO KWA USO NA PADRI
Paparazi wetu alipofika eneo la tukio alikutana uso kwa uso na kiongozi huyo wa kiroho akiwa amesimama kwenye kaburi hilo la Ngwea.
Paparazi wetu alipomfikia Padri huyo alimuuliza kulikoni ndipo alipomsimulia kisa kizima.
“Jana (Alhamisi ya wiki iliyopita) nilioteshwa juu ya kuwepo kwa vitu vibaya kwenye makaburi haya ya waumini wetu ambayo yapo nje ya kanisa letu.
“Nilishtuka sana na kuona mambo ya ajabu, nikaamua kushusha maombi ya kukemea ambapo nilioteshwa kuwepo kwa vitu kwenye makaburi yetu ambayo yako jirani kabisa na sehemu ninayo lala,” alisema Padri Msimbe na kuongeza:
“Leo kulipokucha ndipo nikafika kwenye makaburi haya na kuanza kukagua yote likiwemo la Mangweha (Ngwea) nikayakuta yakiwa na tunguli zilizovishwa sanda ambazo pia zina majina ya waumini wangu wa moja ya vigango vya parokia hii.”

AKATAA KUTAJA MAJINA
Alipoombwa kutaja majina ya waumini hao alisema: “Sitaweza kutaja majina yao wala ya kigango yaliyoandikwa kwani wanajijua wenyewe na mbaya zaidi hata waumini wataona katika ibada Jumapili hii (Jumapili iliyopita), nitaonesha madhabahuni,” alisema padri huyo ambaye tangu alipofika kwenye kanisani hilo limekuwa na maendeleo makubwa.
Kama alivyoahidi, ilipofika Jumapili iliyopita, padri huyo akiwa madhabahuni alisitisha mahubiri kisha akatoa tunguli hizo na sanda na kuwaonesha waumini.
Aliwatangazia waumini hao kuwa vitu hivyo alivikuta kwenye kaburi hilo ambapo alisema kuwa sanda hizo zilikuwa zimeandikwa majina ya baadhi ya wafuasi wa kanisa hilo ndipo kukaibuka hofu hivyo ikabidi maombi ya nguvu yafanyike.
Pamoja na maombi ya nguvu lakini walioona majina ya baadhi waumini wenzao kwenye sanda hizo, walianza kushikwa na mshangao huku wakitazamana usoni.
Paparazi wetu alifikia kwenye ibada hiyo na kujionea jinsi waumini walivyotaharuki kutokana na vitendo hivyo ambavyo vilitokea katika makaburi hayo.
“Mimi hata sielewi maana kwa jinsi ninavyoona, itakuwa kuna watu wasio na hofu ya Mungu wanaendekeza mambo ya kishirikina, sasa wanaandika haya majina lakini najua kwa kuwa tumeyabaini, kwa nguvu za Mungu, watashindwa,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
Paparazi wetu alizidi kutafuta data zaidi juu ya sakata hilo ambapo mwishoni alijiridhisha kuwa tunguli hizo zilipokewa na waumini, zikahifadhiwa katika ofisi ya Padri Msimbe.
Mbali na tunguli hizo zilizokutwa katika kaburi la Ngwea, mwandishi wetu alijionea kiroba cha tunguli hizo zilizozungushiwa  sanda katika ofisi ya padri huyo zilizohifadhiwa chini ya meza.
Minong’ono zaidi ilizidi kuibuka kuwa huenda watu walioweka tunguli hizo kuwa wameweka katika kaburi la Ngwea ili waweze kung’ara kimuziki kama alivyokuwa marehemu.
“Watu wanadanganyana, wamesababisha waumini wengi kuingiwa na hofu juu ya nini hatma yao. Wanaamini mtu anaweza kufariki dunia na mwingine akatembelea nyota yake, tunapaswa kuishi katika matakwa ya kumuamini Mungu siku zote,” alisema muumini mwingine wa kanisa hilo ambaye ni kiongozi kanisani hapo.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya kuifunga Arsenal bao la tano leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London .
Mchezaji wa Arsenal Kieran Gibbs (kushoto) akipewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
CHELSEA imeifanya kitu kibaya Arsenal baada ya kuichapa mabao 6-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England ‘Premiership’, leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Arsenal ambayo iliingia uwanjani katika mechi ya 1,000 tangu kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger alipoanza kuinoa timu hiyo, imekutana na kipigo hicho lakini kukatokea tukio la kushangaza la kadi nyekundu.
Mabao ya Chelsea kwenye mchezo huo yamepatikana kupitia kwa Samuel Eto'o dakika ya 5, Andre Schürrle (7), Eden Hazard (17), Oscar (42 na 66) na Mohamed Salah (71).

Tukio la kushangaza ni kuwa mwamuzi alimpa kadi nyekundu Gibbs wa Arsenal wakati aliyetenda kosa la kuunawa mpira kwa makusudi ni Oxlade-Chamberlain katika dakika ya 15. 
Chelsea Line-up: 1Petr Cech, 2Branislav Ivanovic, 24Gary Cahill, 26John Terry, 28César Azpilicueta, 4David Luiz, 11Oscar,14Andre Schürrle, 17Eden Hazard, 21Nemanja Matic,29Samuel Eto'o
Substitutes: 23Mark Schwarzer, 33Tomas Kalas, 8Frank Lampard, 12John Mikel Obi, 15Mohamed Salah, 9Fernando Torres, 19 Demba Ba

Arsenal Line- up: 1Wojciech Szczesny, 3Bacary Sagna, 4Per Mertesacker, 6Laurent Koscielny, 28 Kieran Gibbs, 7Tomas Rosicky, 8 Mikel Arteta, 9 Lukas Podolski, 5 Thomas Vermaelen, 15 Alex Oxlade-Chamberlain, 19 Santi Cazorla, 12 Olivier Giroud

Substitutes: 21Lukasz Fabianski, 5Thomas Vermaelen, 25Carl Jenkinson, 20Mathieu Flamini, 29Kim Kallstrom, 22Yaya Sanogo,44Serge Gnabry

Picha iliyotolewa na vyombo vya habari vya China vikionyesha kitu kipya kilichogunduliwa na satellite za nchi hiyo kikielea katika Bahari ya Hindi ambacho kinahisiwa huenda kikawa na uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea.
Picha za Satellite kutoka kituo cha utafiti cha Marekani kikionyesha eneo ambako msako mkali unaendelea kuitafuta ndege iliyopotea huko katika bahari ya Hindi.
Hussein aliwaambia waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur: 'Balozi wa China amepokea picha ya kitu kinachoelea kusini mwa bahari ya Hindi na amesema watatuma meli kuchunguza.
Muakilishi wa Waziri Mkuu wa Australia Warren akiongea na waandishi wa habari RAAF Pearce Base.
Ofisa wa anga, Peter Moore, ambaye pia ni rubani, amesema mchanganyiko wa hali ya hewa nchi kavu na ile ya bahari unaathiri ndege za uokoaji.
•    Waziri wa Mawasiliano Malaysia atangaza picha mpya ya Satellite
•    Asema China imetuma meli kuchunguza
•    Ni wiki mbili sasa tokea ndege hiyo ipotee
Kipande kikubwa cha chuma kimeonekana kikielea katika bahatri ya Hindi. Picha za Satellite za China zimeona  kipande chenye urefu wa futi 72 kiasi cha maili 75 mashariki mwa Australia.
Picha hizo zimechukuliwa siku mbili tu baada ya mamlaka za Australia kuona kitu kinachoelea katika pwani ya bahari ya Hindi.
CHANZO NI DAILY MAILY.


Kikosi cha timu ya Yanga SC kilichoanza siku ya leo dhidi ya Rhino Rangers, katika Dimba la Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kikosi cha Rhino Rangers kilichoanza siku ya leo dhidi ya Yanga.
Wachezaji wa Young Africans wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Jerrson Tegete katika Dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Nadir Haroub "Cannavaro" - 23  akipambana na wachezaji wa Rhino Rangers.
Mashabiki wa Rhino Rangers.
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi (kushoto) akiwania mpira na mchezaji waRhino Rangers.
Makocha wa Timu ya Yanga wakiongea jambo.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans, leo wameibuka na ushindi na mabao 3 - 0 dhidi ya wenyeji, timu ya Rhino Rangers katika mchezo uliofanyika jioni katika  Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Yanga iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu jambo ambalo wamefanikiwa na kusogea nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja.
Ikiwatumia washambuliaji wake Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Jerrson Tegete na Emmanuel Okwi safu ya ushambuliaji ya timu ya Young Africans ilikosa mabao kadhaa ya wazi dakika 20 za mwanzo kutokana na ubovu wa uwanja.
Dakika ya 29 ya mchezo Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Rhino kufuatia mpira uliopigwa na Msuva kuokolewa na walinzi wa Rhino kabla ya kumkuta Tegete aliyeukwamisha mpira wavuni.
Timu zote ziliendelea kucheza kwa lengo la kusaka mabao kabla ya mapumziko, lakini mpaka dakika 45 za mchezo zinamalizika, Rhino Rangers 0 - 1 Young Africans.
Kipindi cha pili Young Africans waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya 68 ya mchezo mlinzi wa Rhino Rangers Laban Kambole alijifunga wakati akitaka kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na Msuva na kuifanya timu ya Young Africans kuhesabu bao la pili.
Hussein Javu aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete aliwaiunua mashabiki wa Young Africans dakika ya 90 o kufuatia kuitumia vizuri pasi ya Okwi aliyewatoka walinzi wa Rhino na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamazika, Rhino Rangers 0 - 3 Young Africans.
Baada ya mchezo wa leo Young Africans inafikisha pointi 43 ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Azam FC yenye ponti 44 huku timu zote kwa sasa zikiwa zimecheza michezo 20 na kubakisha michezo sita kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Young Africans: 1. Juma Kaseja, 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub "Cannavaro", 5. Kelvin Yondani, 6. Frank Domayo, 7. Saimon Msuva, 8. Hassan Dilunga, 9. Jerson Tegete/Hussein Javua, 10. Mrisho Ngasa, 11. Emmanuel Okwi 

Friday, March 21, 2014


Stori: waandishi wetu
Kimenuka upyaaa! Wale mashostito wawili katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja ambao walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana, wanadaiwa kuvunja rasmi ushosti wao, Ijumaa limenyetishiwa.
http://api.ning.com/files/D7OtuoxqP96Ie2CpOEMa26JChvSpjMbvCLdqbDauoujND4ZjSnKnoreWn2q1Akwr01dD9qV7a04IWu0d0i2qVgSjuwGf5msX/wemanakajala.JPG
Wema na Kajala wakiwa bado mashosti.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki wa mastaa hao, hivi sasa hali ni tete huku sababu mbalimbali zikidaiwa kuwa chanzo cha yote.
WEMA KARUDI KWA SNURA?
Chanzo hicho kilidai kuwa kila mmoja kwa sasa amechukua hamsini zake huku Wema akidaiwa kurudi kwa shostito wake wa zamani, mamaa wa Majanga, Snura Mushi.
KISA CHA SALUNI
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa chanzo kikubwa ni kuwa mashosti hao walikutana katika saluni moja maarufu iliyopo Kinondoni, Dar ambapo Kajala alikuwa akitokea kwenye ‘shutingi’ ya filamu yake.
Ilidaiwa kuwa Kajala alifika saluni hapo akiendesha baiskeli iliyosababisha akaloa jasho sehemu kubwa ya mwili wake.
Ilisemekana kwamba Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini Kajala alimkwepa kwa sababu mwili wake ulikuwa na jasho jingi, jambo lililomfedhehesha Wema na kununa.
“Yaani baada ya Kajala kukwepa kukumbatiwa, Wema aliumia sana.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo hicho.
Wema akiwa na Kajala baada ya kumnusuru kwenda gerezani.
KISA CHA NYUMBANI
Hata hivyo, chanzo kingine kilicholonga na Ijumaa kilidai kwamba kuna siku Kei alikwenda nyumbani kwa Wema, Kijitonyama Dar kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia sinema).
DIAMOND ANANYIMA FURSA?
Ikadaiwa kuwa Kajala alipofika nyumbani hapo aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo amelala na Diamond na huwa hawaamshwi.
Chanzo hicho kilidai kwamba Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu na akamwambia asubiri ambapo msanii huyo alisubiri kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.
Pia chanzo hicho kilitiririka kwamba ushosti wa Wema na Kajala ulianza kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond mara baada ya kurudiana na Wema.
KIVIPI?
Chanzo hicho kilinyetisha madai kwamba eti Kajala hampendi Diamond kwani jamaa huyo amekuwa akitumia muda mwingi kuwa na Wema hivyo kubana fursa ya mashosti hao kujiachia.
“Unajua kabla Diamond hajarudiana na Wema, Kajala alikuwa anaweza kufika pale kwa Wema na kuingia hadi chumbani kwa shosti wake lakini sasa inashindikana kwa sababu anakuwepo Diamond,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Ndiyo maana Kajala ameona kama mbwai, mbwai tu! Kila mtu afe kivyake.”
HUYU HAPA KAJALA
Kwa upande wake Kajala alipopatikana, awali hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai kuwa hana tatizo na Wema na kwamba sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Alipotafutwa Wema na kusimuliwa mkasa mzima alisema kwa kifupi: “Mimi niko sawa, hakuna kitu na muda si mrefu watu watatuona tena pamoja,” alisema Wema.
SI MARA YA KWANZA
Wema na Kajala wamekuwa mashosti wa muda tangu Wema alipomlipia mwenzake faini ya Shilingi Mil. 13 mahakamani na kumuepusha kwenda jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kutibuana kwani mwaka jana waligombana lakini baadaye wakapatana.


StoriMwandishi wetu
WAKATI masuala ya ushoga yakipingwa kwa nguvu zote hapa nchini, skendo ya aina yake imeikumba serikali baada ya siri kuvuja kuwa mmoja wa viongozi kumi wa juu nchini ni shoga.
Taric Jumbe akitoa ushuhuda jinsi alivyofanya mapenzi na kigogo huyo.
Habari hizo za kushtua na kufedhehesha taifa ambazo zimefanyiwa kazi na dawati la Ijumaa kwa kushirikiana na kitengo cha OFM cha Global, zilitua hivi karibuni chumba cha habari kupitia kwa kijana aliyejitokeza na kueleza alivyofanya mapenzi ya jinsia moja na kigogo huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa.
KIJANA HUYO NI NANI?
“Mimi naitwa Taric Jumbe, nina miaka 21, nimefika hapa kutoa ushuhuda wangu kuwa nilifanya mapenzi na... (anataja jina), tulianza kuchat kwenye Facebook, akaniomba urafiki, nikamkubalia nikijua ni wa kawaida tu.
“Baadaye akaanza kunitongoza na kuniahidi fedha nyingi, nikakubali. Siku ya kwanza tulikutana Dar, Hoteli ya Serena, akanielekeza chumba alichopo (anataja namba ya chumba), nikaenda na kuwakuta walinzi wake, nilipojitambulisha wakaniruhusu kuingia chumbani kwake. Nimeshafanya naye mara tatu,” alisema kijana huyo.
JINSI WALIVYOWASILIANA
Mbali na matumizi ya mtandao wa kijamii, wanahabari wetu walitaka kujua mpaka kijana huyo anafika hotelini hapo, alikuwa akiwasiliana na kigogo huyo kwa njia gani? Jumbe akasema:
“Mwanzo nilikuwa nawasiliana naye kwa Facebook lakini tulipozoeana alinipatia namba zake za simu.”
Jibu hilo lilitoa mwanya kwa makachero wa gazeti hili kuperuzi mtandao wa simu ile ili kujua kama anayeitumia namba hiyo ni kigogo huyo au ni changa la macho.
Bila chenga ilibainika kuwa namba hiyo ni ya kigogo huyo, lakini ilipopigwa kwa lengo la kuwasiliana naye moja kwa moja, iliita bila kupokelewa na kuwafanya waandishi kuendelea na kazi ya kumhoji kijana huyo kwa kina.
Taric akiwa ndani ya Global kuelezea sakata hilo la kufanya mapenzi na kigogo serikalini.
KUHUSU MALIPO
Jumbe aliweka wazi kuwa siku ya kwanza kukutana naye alilipwa shilingi elfu themanini sambamba na ahadi kuwa wakati wowote atakapokuwa na shida awasiliane na kigogo huyo ambaye msafara wake huongozwa na pikipiki yenye king’ora na gari la polisi, kwa lengo la kuwezeshwa kimaisha.
Aliongeza kuwa kiasi kikubwa alichowahi kuhongwa ni shilingi laki tatu (300,000), huku akiainisha kwamba fedha nyingine alikuwa akipewa kidogokidogo kwa ajili ya kujikimu.
MSHANGAO MWINGINE
Mbali na kijana huyo kukiri kufanya mapenzi mara mbili na kigogo huyo hotelini, mshangao ulikuja pale alipoweka wazi kuwa mara ya tatu alimfuata kiongozi huyo nyumbani kwake ambako alishirikiana naye tendo hilo la aibu.
Waandishi walipotaka kujua waliwezaje kufanya uchafu huo nyumbani kwa kigogo huyo mwenye familia, Jumbe alisema: “Ni kweli anaishi na familia lakini nje ya nyumba yake ana ofisi, huko ndiko alikonikaribisha na kunifanyia mchezo huo.”
UPEKUZI WA MAWASILIANO
Baada ya maelezo hayo, waandishi wetu waligeukia uchunguzi wa mawasiliano ya simu na mtandao wa Facebook baina ya Jumbe na kigogo huyo ambapo walibaini kuwepo kwa mambo ya aibu kubwa.
Kwa macho maangavu, waandishi wetu walioneshwa meseji alizokuwa akituma kigogo huyo ambazo chache kati ya hizo zilisomeka: “Baby, mke wangu, honey,” huku Jumbe naye akichagiza majibu kwa mtindo huohuo hadi naye kufikia mahali pa kumwita kigogo huyo ‘mume wangu’, aibu iliyoje!
Kama hiyo haitoshi, wawili hao walifikia hatua ya kusifiana namna walivyoumbika na kupeana mapenzi motomoto na kuahidiana kuwa pamoja milele. Kufuru kubwa kwa Muumba!
WIVU HAUKUKOSEKANA
Katika hali ya kustaajabisha na kuonesha kuwa kigogo huyo amekubuhu kwenye mambo hayo, wakati mwingine akiwa nje ya nchi alidiriki kumuonea wivu kijana huyo ambapo mara kadhaa alituma meseji ya kutishia kumwacha kutokana na kile alichokiita ‘kutoka nje ya ndoa’.
Moja kati ya meseji hizo za fedheha kutoka kwa mheshimiwa huyo, ilimtuhumu Jumbe kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine, jambo ambalo kijana huyo alilikanusha na wote kuwekana sawa kwa lengo la kusonga mbele na uhusiano wao.
KIGOGO MZITO AHOJIWA
Baada ya kupata maelezo hayo ya kutisha na kusikitisha, kwa zaidi ya mwezi mzima, gazeti hili lilifanya juhudi za kumtafuta kigogo huyo ili kuweza kupata maelezo yake kuhusiana na mkasa huo.
Hatimaye, kwa namna ya kijasusi, Ijumaa liliweza kumfikia na kummwagia data zote, zikiwemo picha za kijana huyo na nakala ya mawasiliano katika mtandao wa Facebook ambapo alionekana kuduwaa.
Hata hivyo, kutokana na waandishi wetu kufanya mahojiano na kigogo huyo huku wapambe wake wanaomlinda na kumuongoza wakiwepo, haikuwezekana kufungua kila kitu wazi kwa vile mazungumzo hayo yalikuwa yakirekodiwa.
Baada ya kuoneshwa tuhuma zake kwa kutumia nyaraka, mheshimiwa huyo alikiri: “Nazifahamu hizi nyaraka.” Akimaanisha alichokiona kinamhusu kwa asilimia mia moja.
TAHADHARI
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa tumeamua kulificha kwa makusudi jina la kigogo huyu ili kuilinda heshima yake ambayo ni kubwa katika jamii yetu. Tutaliweka wazi wakati wowote endapo kati ya mambo haya yatajitokeza.
Mosi, kijana huyo (Jumbe) atadhuriwa. Tunajua nguvu alizonazo mheshimiwa huyu ni kubwa, tunaomba kumfahamisha kwamba tutamuanika hadharani endapo Jumbe atafikwa na matatizo yoyote yasiyo ya kawaida.
Pili, endapo tutathibitisha kuwa anaendelea na mchezo wake huu usiokubalika na mwisho, endapo waandishi waliokwenda kufanya naye mahojiano, ambao yeye na wapambe wake wanawafahamu, watapata madhara yoyote


Pichani juu ni taswira za sehemu ya Hoteli ya Pecolo Beach iliyopo Kawe jijini Dar iliyoteketea kwa moto leo mchana. Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye nguzo iliyopo jirani na hoteli hiyo.