Tuesday, February 18, 2014

Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
Yelewiii!  Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na changudoa  ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.
Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.
OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti’ namba upande wa  mbele) mali ya kampuni  hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na kupaki gari  kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.
Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru dereva  ashuke.
Hata hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya gari.
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa naye.
Akizungumza kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.
Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake (Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili.
Stori: Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana kwa jina moja la Nagar.
Estelinah Sanga 'Linah'.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi, ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema bila kufafanua zaidi.
KWA MARA YA KWANZA MSHINDI  KWENDA KUIWAKILISHA USA KWENYE MASHINDANO YA REDD'S MISS TANZANIA  2014 - JIJINI DAR-ES-SALAAM
MSHINDI WA 1,2,3 KILA KANDA KUJA DC KWENYE FINALS AMBAPO
MKURUGENZI NA MWAKILISHI WA MISS TANZANIA KUTOKA TANZANIA WATAKUWEPO KUTOA TAJI HILO.
MSHIRIKI LAZIMA AWE NA MAKARATASI YA KUSAFIRIA
VENUES & REGISTRATION -DROPPING NEXT 
MAELEZO-TUANDIKIE ## MISSTANZANIA2014@GMAIL.COM
DSC_0851
Mwezeshaji wa warsha hiyo ambaye pia ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa utambulisho kwa waendesha warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kutoka Shirika la Search for Common Grounds (SFCG), yanayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0006
Meneja Mradi wa SFCG wilaya ya Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akielezea maudhui ya warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao ni waandishi wa redio za jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inafanyika mjini Dodoma.
DSC_0016
Washiriki wa warsha wakimsikiliza Bw. Jacob Mulikuza kutoka Shirika la Search for Common Grounds – SFCG (hayupo pichani) akielezea jambo wakati wa warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro inayoendelea mjini Dodoma kwa waandishi na watangazaji wa Redio za Jamii nchini iliyofadhiliwa na UNESCO kupitia mradi wa DEP.
DSC_0018
DSC_0023
Mmoja wa washiriki akifafanua jambo katika warsha hiyo iliyojadili namna ya kuandika habari za migogoro kutoka Shirika la Search for Common Grounds (SFCG) yanayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0082
Meneja mradi wa SFCG wilaya ya Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akiwapatia maelekezo washiriki wa warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kuhusu namna ya uwajibikaji katika kutatua migogoro ndani ya Jamii.
DSC_0076
Mmoja wa washiriki Bwana Baraka kutoka ORS Fm Radio, akiwaelezea washiriki wenzaka namna Ya kutatua fumbo lililokuwa sehemu ya kazi za Vikundi, katika warsha ya Uandishi wa habari za Migogoro kuhusu namna ya uwajibikaji katika kutatua migogoro ndani ya Jamii.
DSC_0105
Mratibu wa vyombo vya habari wa SFCG Zanzibar, Bwana Ali sultan, akielezea kuhusu ushiriki wa SFCG huko Zanzibar katika warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao ni waandishi wa Redio za Jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inayofanyika mjini Dodoma imefadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani (DEP) kuelekea Uchaguzi 2015.
DSC_0115
Meneja Mawasiliano wa SFCG kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bwana Dupont Ntererwa, akielezea kuhusu ushiriki wa SFCG huko DRC katika warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao ni Waandishi wa Redio za Jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inayofanyika mjini Dodoma.
DSC_0156
Washiriki wakifanya kazi za vikundi.

Monday, February 17, 2014

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAJANGA! Siku chache baada ya hivi karibuni kudaiwa kunywa sumu, staa mkubwa wa sinema Bongo, Wastara Juma amepata tena ajali mbaya.
Wastara Juma.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti namba wani la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita zilieleza kuwa siku ya tukio Wastara alitoka nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar na gari lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili ya kwenda kununua umeme.
Akizungumzia tukio hilo kwa masikitiko, Wastara aliliambia gazeti hili kuwa kabla ya kufika kwenye kituo cha kununulia umeme (Luku) alikutana na lori kubwa lililokuwa kwenye mwendo kasi huku likiwa limewasha taa fulu.
Gari aina ya Toyota Vitz alilopata nalo ajali Wastara.
Alisema kuwa alijaribu kulikwepa lakini lilimsukuma na kujikuta akiingia mtaroni kutokana na barabara kuwa nyembamba ambapo aliumia sehemu za kichwani na mguuni kwa ndani.
Wastara alisema baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya TMJ, Dar ambapo alisafishwa majeraha (dressing) kisha akapatiwa matibabu na baadaye aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nimenusurika kifo, namshukuru sana Mungu kwani ajali ilikuwa mbaya nilihamishwa kwenye siti niliyokuwa nimekaa na kurushwa kwenye siti nyingine huku nikijigonga na kuumia kichwani.
“Pia gari langu limeharibika sana, kioo chote kimevunjika, sielewi kwa nini haya yote yananitokea.
“Namuomba Mungu anisaidie maana naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo na kwa nguvu zangu mwenyewe siwezi,”alisema Wastara.
Hata hivyo, Wastara kwa sasa anaendelea vizuri japokuwa bado anaumwa kichwa na mguu.
Wastara ameshapata ajali mara kadhaa ikiwemo ile ya pikipiki aliyopata mwaka 2008 akiwa na aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Pia aliwahi kupata nyingine ya gari akiwa na Sajuki.
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Wastara, kuna watu wanamtakia mabaya ili amfuate Sajuki aliyefariki Januari 2, mwaka jana.
Staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' pamoja na Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' wakipitia Gazeti la Ijumaa Wikienda ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati wakisubiri kusikiliza kesi inayomkabili Lulu juu ya kifo cha msanii Steven Kanumba.
 Elizabeth Michael 'Lulu' (katikati) akiwa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila (wa pili kushoto) na Dk. Cheni (kulia) ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Na Waandishi wetu
KESI inayomkabili staa wa sinema za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ dhidi ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba imeunguruma leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku mtuhumiwa akikiri baadhi ya mashtaka.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo watakapojulishwa na mahakama tarehe ya kusomwa kwa shitaka lake la kuua bila kukusudia.
Habari kamili kuhusu kesi hiyo Soma Gazeti la Risasi Jumatano.
(Imeandikwa na Jelard Lucas, Haruni Sanchawa / GPL)
Msanii Zuwena Mohammed 'Shilole' Februari 13, mwaka huu alimtembelea mama yake mlezi aitwaye Hamisa anayeishi Igunga Mjini mkoani Tabora alipokwenda na wasanii wenzake akina Madee na Queen Darleen kwa ajili ya shoo ya Siku ya Wapendanao.(Video na Denis Mtima / GPL, Igunga)

Stori: Haruni Sanchawa
BUNGE la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza leo na tayari wajumbe wa bunge hilo wamewasha moto wa mjadala hata kabla ya vikao rasmi kuanza.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili juzi walisema mijadala inayotarajiwa kuzusha malumbano makubwa ni suala la muundo wa muungano ambapo kuna baadhi yao wanaungana na Tume ya Jaji Joseph Warioba ambayo imependekeza kuwepo na serikali tatu huku wengine wakitaka serikali mbili au moja.
Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bunge hilo amesema wazi kuwa ikiwa suala la Tanganyika litazimwa, atajiuzulu ujumbe na kwenda mahakamani.
“Kuna watu wenye msimamo wa vyama na wajumbe wengi hawataweza kutetea hoja… wanakwenda bungeni wakiwa na maelekezo ya nini cha kufanya huku wengine wakiwa hawajui                wala hawaielewi rasimu,” alisema Mtikila.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amesema anaamini rushwa itatumika kushinikiza wajumbe wa Bunge la Katiba kupitisha masuala mbalimbali.
“Nawashauri wabunge kutoacha kupokea bahasha watakazopewa lakini wasisahau majukumu yao kwa taifa,” alisema Makinda.
Alifunguka kuwa katika Bunge hilo kutakuwa na makundi mbalimbali ambayo yatatumia nguvu nyingi ili kuweza kupitisha mambo wanayoyataka ili yawepo katika katiba.Bunge hilo litaketi kwa siku 90.


Chris (kushoto) na Mohsin wakipata 'moja moto moja baridi' na pichani chini ni wake zao.
Kila mmoja na mpenzi wake alisherekea Siku Kuu ya Wapendanao (Valentine's Day) kwa staili yake, wakiwemo Mzee wa Kazi Chris Lukosi na Bw. Mohsin ambao wao waliamua kutoka na wake zao na kwenda kula bata kiwanja cha CLUB GUVNOR LONDON kama wanavyoonekana pichani.
PICHA: Mdau wetu wa London, Uingereza

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji  la  Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi.
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo  mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.


NIMSHUKURU sana Mungu, muumba wa mbingu na ardhi kwa kuweza kutufikisha tena leo, kama alivyofanya jana, juzi na kila siku bila ya sisi kutumia gharama yoyote. Vitendo vyake kwetu ni vya utukufu mkuu, ingawa mara nyingi binadamu tumekuwa tukifanya vitu vingi vya kumkwaza.
Jaji Joseph Sinde Warioba.
Baada ya kusema maneno hayo, naomba sasa niende kwenye hoja yangu ya leo, ambayo kwa hakika ni ya msingi sana kama bado tunataka kujenga taifa lenye mshikamano, uimara na lisilo na mgawanyiko, kwa misingi ya kabila, dini wala rangi.
Wote tunajua kwamba leo, Bunge maalum la Katiba linaanza vikao vyake mjini Dodoma, likiwa na lengo moja tu, kupata katiba bora kabisa ambayo nchi yetu itaifuata kwa ajili ya ustawi wake na wananchi.
Hii ni baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Marekebisho ya Katiba, iliyoratibu maoni ya wananchi nchi nzima, iliyofanya kazi chini ya Uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu wake, Jaji Augustino Ramadhan.
Ingawa kumekuwa na kutokuelewana kwa hapa na pale miongoni mwa wanasiasa kuhusiana na mchakato huo, ni jambo la kushukuru kwamba hadi sasa, tunapoelekea bungeni, tumeweza kuvumiliana na kukubaliana juu ya mambo ya msingi kwenye katiba yetu.
Hata hivyo, wakati tukielekea katika hatua hii kubwa na muhimu zaidi, zipo dalili zinazoonyesha kwamba kutakuwa na mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe juu ya mambo mbalimbali. Kinachotia shaka, ni baadhi ya vitu ambavyo havionyeshi kama wajumbe hao wako makini na ustawi wa nchi yetu au la.
Ni kwa kutambua umuhimu wa kuiweka mbele nchi yetu kabla ya kitu chochote, ningependa kuwashauri wajumbe wetu kutumia zaidi busara katika mijadala yao ili historia iweze kuandikwa, vinginevyo, tunaweza kujikuta tukizalisha katiba ambayo italeta janga kwa taifa badala ya heri kama ilivyo matarajio ya kila mmoja.
Endapo kila mmoja atalazimisha kupita kwa hoja au mawazo yake, basi ni bora tukasitisha mchakato huu, ili tuufanye kwa utaratibu mwingine bora zaidi, mradi tu mwisho wa siku, iwe ni Tanzania ndiyo iliyofaidika na katiba hiyo, badala ya vyama vya siasa au asasi za kiraia zenye wajumbe wake katika bunge hilo.
Ni lazima tuelewe kuwa siyo kila hoja ya kila mjumbe itapitishwa, zipo zitakazoachwa au kuboreshwa. Wajumbe wetu lazima watazame zaidi faida ya hoja kwa taifa badala ya vyama vyao vya siasa au taasisi wanazoziwakilisha.
Kinachoonekana ni kuwa baadhi ya wajumbe hao, kwa kutotambua kwamba umuhimu wa taifa letu kuwekwa mbele, wamekwenda Dodoma wakiwa na katiba yao, kwamba ni kile tu wanachotaka wao ndicho kinachotakiwa kuwemo ndani yake.
Hii siyo sawa. Kama italazimu, ni bora kama watakubaliana katika kutokukubaliana na zoezi hilo likaahirishwa hadi wakati mwingine, mradi tu, lengo linafikiwa. Itakuwa ni kuwasaliti wananchi, kama wajumbe wetu watakubali kulazimisha kupitisha jambo ambalo wanajua wazi kabisa, halina masilahi kwa wananchi na taifa kwa ujumla wake.
Katiba ni jambo nyeti, tusilipeleke ili mradi tu tumefanya, isipokuwa tulifanye kwa weledi na mapenzi makubwa kwa nchi yetu, kwa sababu tunajua kwamba suala hili linatuhusu sisi tuliopo hivi sasa na vizazi vyetu vijavyo. Tusije kutenda jambo ambalo watoto na wajukuu zetu wakaja kutulaumu hapo baadaye.
Tanzania ni bora zaidi kuliko chama chochote cha siasa, kwa sababu tunaweza kupoteza chama chochote tukaunda kingine, lakini tukiipoteza Tanzania, kamwe hatutaweza tena kuipata popote.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.


Stori: Makongoro Oging’
MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi  wa Kijiji cha  Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa  mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba.
Mtoto Ismail Barihegi.
Barihegi ambaye amelazwa katika Jengo la Mwaisela Wodi na 17, Muhimbili, alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba siku ya tukio (hakumbuki)alikuwa akichunga ng’ombe porini lakini ghafla walitokea watu  na kumwuliza kwa nini aliwaachia ng’ombe wake kufika shambani.
Alisema aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani haikuwa ya kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
“Wenye ng’ombe walishakimbia, waliniambia ni lazima waniue, niliwaomba wasiniue, lakini hawakunijali, niliishiwa nguvu, damu nyingi ilikuwa imenitoka,waliondoka na kuniacha porini peke yangu.
“Nilipiga kelele ili nipate msaada lakini hakuna aliyejitokeza, nilikata tamaa, baada ya saa kadhaa mtu mmoja alipita na kuniona, akawaita watu akiwemo Mwenyekiti wa kijiji chetu, wakaja kunichukua na kunikimbiza katika zahanati,” alisema mtoto huyo.
Kijana huyo alisema kwamba baada ya huduma ya kwanza katika zahanati hiyo, alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuonekana mbaya zaidi na kwamba ana uhakika wazazi wake hawajui alipo kwani hadi sasa hawajafika kumtembelea.
“Ninamshukuru sana mwenyekiti kwa kunipa msaada mkubwa, sasa hivi amerudi kijijini, najua atawapa taarifa ndugu zangu, ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa kuokoa maisha yangu kwani kwa sasa nina nafuu tofauti na nilivyookotwa katika msitu mnene,” alisema Barihegi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Athumani mtasha alipoulizwa kuhusiana na tukio alisema kuwa amehamishiwa makao makuu.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP Urich matei yupo nje ya mkoa kikazi ila kaahidi kufuatilia sakata hilo kwa undani.