Monday, February 17, 2014


Stori: Haruni Sanchawa
BUNGE la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza leo na tayari wajumbe wa bunge hilo wamewasha moto wa mjadala hata kabla ya vikao rasmi kuanza.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili juzi walisema mijadala inayotarajiwa kuzusha malumbano makubwa ni suala la muundo wa muungano ambapo kuna baadhi yao wanaungana na Tume ya Jaji Joseph Warioba ambayo imependekeza kuwepo na serikali tatu huku wengine wakitaka serikali mbili au moja.
Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bunge hilo amesema wazi kuwa ikiwa suala la Tanganyika litazimwa, atajiuzulu ujumbe na kwenda mahakamani.
“Kuna watu wenye msimamo wa vyama na wajumbe wengi hawataweza kutetea hoja… wanakwenda bungeni wakiwa na maelekezo ya nini cha kufanya huku wengine wakiwa hawajui                wala hawaielewi rasimu,” alisema Mtikila.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amesema anaamini rushwa itatumika kushinikiza wajumbe wa Bunge la Katiba kupitisha masuala mbalimbali.
“Nawashauri wabunge kutoacha kupokea bahasha watakazopewa lakini wasisahau majukumu yao kwa taifa,” alisema Makinda.
Alifunguka kuwa katika Bunge hilo kutakuwa na makundi mbalimbali ambayo yatatumia nguvu nyingi ili kuweza kupitisha mambo wanayoyataka ili yawepo katika katiba.Bunge hilo litaketi kwa siku 90.

0 comments:

Post a Comment