Tuesday, March 18, 2014


Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Ponda akiteta jambo na askari Magereza.
...Akiwa na mwanasheria wake.
...Akitolewa nje ya mahakama.
Afisa  magereza na polisi wakijadili jambo nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Ulinzi ulivyokuwa mahakamani.
Sheikh Ponda akiingizwa kwenye basi.
Afisa wa polisi akifanya mawasiliano kuimarisha ulinzi.
Wafuasi wa Ponda  wakiwa mahakamani.
Polisi wakiwa wamedhibiti barabara wakati wa kuondoka kwa Shehe Ponda.
Wakili wa Ponda, Juma Nassoro, akifanya mahojiano na wandishi wa habari nje ya mahakama.
Ombi la marejeo lililowasilishwa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaamilipotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria.
Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji Augustine Mwarija.
Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment