Thursday, March 13, 2014


Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Jacqueline Wolper.
Jack Wolper, Marry na Tiko wakipata msosi.
Wasanii wakijiachia baada ya kikao.
Mzee Chillo na Wolper wakibadilishana mawazo.
Viongozi wa Bongo Muvi Steve Nyerere, Cloud na William Mtitu katika pozi.
  Mama Rolaa akipata msosi kwenye utambulisho huo.
Steve akifafanua jambo.
Wastara naye alikuwepo.
MABIBO beer, wines and spirits Ltd, waaagizaji na wasambazaji wa kinywaji cha Windhoek Tanzania, ndiyo mdhamini mkuu wa maadhimisho ya kutimiza miaka mitatu ya Bongo Movies yanayotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu.
Mdhamini huyo ametambulishwa leo na Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere katika ukumbi uliopo ndani ya jengo la Arcade, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi kwenye ofisi hizo, Steve baada ya kumtambulisha mdhamini huyo, alisema kuwa wamepania kufanya mambo makubwa siku hiyo kwani kutakuwa na uchaguzi wa balozi wa kinywaji hicho kimataifa pamoja na utoaji tuzo za heshima kwa waliotangulia mbele ya haki.
Aidha aliongeza kuwa, siku  hiyo kutakuwa na wasanii mbalimbali watakaosindikiza maadhimisho hayo wakiwemo Banana Zorro, Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma na wengine wengi huku kiingilio kikiwa shilling 10,000/= Viti vya kawaida na 50,000/= kwa VIP.
Tiketi za maadhimisho hayo zitaanza kuuzwa siku tatu kabla kwenye Klabu ya East 24 iliyopo Mikocheni B, Dar.

0 comments:

Post a Comment