Saturday, March 22, 2014


Kikosi cha timu ya Yanga SC kilichoanza siku ya leo dhidi ya Rhino Rangers, katika Dimba la Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kikosi cha Rhino Rangers kilichoanza siku ya leo dhidi ya Yanga.
Wachezaji wa Young Africans wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Jerrson Tegete katika Dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Nadir Haroub "Cannavaro" - 23  akipambana na wachezaji wa Rhino Rangers.
Mashabiki wa Rhino Rangers.
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi (kushoto) akiwania mpira na mchezaji waRhino Rangers.
Makocha wa Timu ya Yanga wakiongea jambo.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans, leo wameibuka na ushindi na mabao 3 - 0 dhidi ya wenyeji, timu ya Rhino Rangers katika mchezo uliofanyika jioni katika  Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Yanga iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu jambo ambalo wamefanikiwa na kusogea nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja.
Ikiwatumia washambuliaji wake Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Jerrson Tegete na Emmanuel Okwi safu ya ushambuliaji ya timu ya Young Africans ilikosa mabao kadhaa ya wazi dakika 20 za mwanzo kutokana na ubovu wa uwanja.
Dakika ya 29 ya mchezo Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Rhino kufuatia mpira uliopigwa na Msuva kuokolewa na walinzi wa Rhino kabla ya kumkuta Tegete aliyeukwamisha mpira wavuni.
Timu zote ziliendelea kucheza kwa lengo la kusaka mabao kabla ya mapumziko, lakini mpaka dakika 45 za mchezo zinamalizika, Rhino Rangers 0 - 1 Young Africans.
Kipindi cha pili Young Africans waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya 68 ya mchezo mlinzi wa Rhino Rangers Laban Kambole alijifunga wakati akitaka kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na Msuva na kuifanya timu ya Young Africans kuhesabu bao la pili.
Hussein Javu aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete aliwaiunua mashabiki wa Young Africans dakika ya 90 o kufuatia kuitumia vizuri pasi ya Okwi aliyewatoka walinzi wa Rhino na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamazika, Rhino Rangers 0 - 3 Young Africans.
Baada ya mchezo wa leo Young Africans inafikisha pointi 43 ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Azam FC yenye ponti 44 huku timu zote kwa sasa zikiwa zimecheza michezo 20 na kubakisha michezo sita kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Young Africans: 1. Juma Kaseja, 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub "Cannavaro", 5. Kelvin Yondani, 6. Frank Domayo, 7. Saimon Msuva, 8. Hassan Dilunga, 9. Jerson Tegete/Hussein Javua, 10. Mrisho Ngasa, 11. Emmanuel Okwi 

0 comments:

Post a Comment